Aliyewafunga Yanga Hat Trick Atoweka

 

Kikosi cha timu ya Stand.

YULE straika wa Stand United aliyeweka rekodi ya kuwafunga Yanga mabao matatu ‘hat trick’, Alex Kitenge, raia wa Burundi, ametoweka kwenye kikosi hicho na kufunguka kuwa hali ngumu inayoikumba timu hiyo ndiyo chanzo cha yeye kujiengua kwenye klabu hiyo na hana mpango wa kurejea klabuni hapo kwa sasa.

 

Kitenge anashikilia rekodi ya kuwafunga Yanga mabao matatu licha ya timu yake kupoteza kwa mabao 4-3 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa mwanzoni mwa msimu huu na kusababisha Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kutamka kuwa ni mmoja wa wachezaji bora ambao alitamani kuwaongeza kwenye kikosi chake.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kitenge alisema kwa sasa yupo kwao Burundi akijaribu kuangalia
mustakabali mwingine baada ya kuyashindwa maisha katika kikosi cha Stand United kwa kuwa amekuwa akicheza bila kulipwa kwa muda mrefu na kufanya aishi maisha magumu.

 

“Nipo Burundi rafiki yangu, hapo Stand nimeondoka kidogo kwa sababu maisha ambayo tunaishi ni magumu sana kwa sababu tumekuwa tukicheza bila kulipwa kwa muda mrefu sana, mwenyewe unajua kuwa maisha ya sasa yanahitaji fedha ili uweze kuishi vizuri, kwa hiyo sijajua ni lini nitarudi klabuni hapo,” alimaliza Kitenge.

Loading...

Toa comment