Amber Rutty: Jela Siyo Pa Mchezomchezo, Pasikie tu

Video Queen, Mascat Abubakary ‘Amber Rutty’ (katikati).

KWA mara ya kwanza tangu atoke gerezani kwa dhamana, Video Queen, Mascat Abubakary ‘Amber Rutty’ ameibuka na kueleza kuwa jela siyo pa mchezomchezo, watu wapasikie tu.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Amber Rutty alisema maisha ya jela siyo mazuri ndiyo maana tangu atoke kwa dhamana amekuwa na matatizo ya kiafya na kisaikolojia.

Aliendelea kusema kuwa kwa sasa hajawa sawa kwa ajili ya kuelezea kiundani kuhusu alichojifunza huko jela kwani hali yake bado haijatengamaa akirudi katika hali yake ya kawaida ataeleza mengi lakini kifupi watu watambue kuwa jela siyo mahali pazuri hivyo wawe makini.

“Kiukweli tangu nimetoka jela nimekuwa nikiumwa sana, yaani afya yangu siyo nzuri ndiyo maana sijaweza hata kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na maswali yao wanayohitaji kujua kutoka kwangu. Alipohojiwa nini kinamsumbua katika afya yake, Amber Rutty alikuwa na haya ya kusema: “Pamoja na ukweli kuwa afya yangu siyo nzuri pia kisaikolojia siko sawa hivyo nikiwa vizuri ndiyo nitaongea mengi,” alisema Amber Rutty.

 

Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao bado inaendelea kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu sasa wako nje kwa dhamana.

Kabla ya dhamana hiyo, wawili hao walisota katika Gereza la Segerea kwa siku 25.


Loading...

Toa comment