Stars Ikifuzu Kuibukia Kwa Misri

KUNA kila dalili kwamba Taifa Stars ikimfunga Uganda Machi 3 mwakani, itafuzu kwa fainali za Afcon ambazo zina nafasi kubwa ya kufanyika Misri badala ya Morocco na Afrika Kusini. Stars inahitaji ushindi kwenye mchezo huo huku ikiombea Cape Verde atoke sare na Lesotho nyumbani au kushinda mechi hiyo.

 

Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra inazo ni kwamba Januari 9, Misri ana nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa mwenyeji wa Afcon baada ya Cameroon kupigwa chini.

 

Ingawa Afrika Kusini nao wanawania nafasi ya kuandaa fainali hizo sawa na Morocco lakini Misri inapewa nafasi kubwa mpaka sasa kwakile kilichoelezwa kwamba miundombinu yao ipo tayari. Mmoja wa vigogo wa Caf, Amaju Pinnick alisema watazingatia kigezo cha nchi iliyo tayari kimiundombinu kwavile muda uliobaki ni mchache.

Loading...

Toa comment