Mafaili Ya Waarabu Yakabidhiwa Kwa Mo

Mohammed Dewji ‘Mo’

WAKATI Simba wakipambana na Waarabu JS Saoura, kesho Jumamosi tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji amepeleka faili zima la Waarabu hao kwa ‘big boss’, Mohammed Dewji ‘Mo’.

 

Simba inatarajia kushuka dim­bani kesho Jumamosi kuvaana na JS Saoura kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa kwanza wa Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki katika hatua hiyo.

 

Simba ipo Kundi D sambamba na timu za Al Ahly ya Misri na AS Vita ya DR Congo.

 

Taarifa ambazo Championi Ijumaa, imezipata kutoka Simba zinasema kuwa, katika ripoti hiyo ya Aussems aliyoikabidhi kwa Mo hivi karibuni ameweka mikakati yake kuelekea hatua ya makundi ikiwa ni pamoja na kuwaondoa Waarabu katika mchezo huo.

 

“Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilikutana hivi karibuni kujadili ripoti ya kocha kuhusiana na mechi za ligi na michuano ya kimataifa ambapo ripoti hiyo ilieleza juu ya mikakati yake ya kuifikisha Simba hatua ya makundi.

 

“Lengo kubwa ni kuhakikisha tu­na­chukua pointi zote tisa za nyumbani kwa kuanza na mechi ya Jumamo­si dhidi ya Waarabu JS Saoura ambapo tunahitaji kutua hatua ya makundi,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Simba imefaniki­wa kutinga hatua ya makundi baada ya kui­funga Mbabane Swallows ya Eswatini kwa kuichapa jumla ya mabao 8-1 ikiwa ni pamoja na kui­ondoa Nkana FC ya Zambia kwa mabao 4-3 hatua ambayo imewafurahi­sha viongozi hao.

Stori na Khadija Mngwai,

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment