The House of Favourite Newspapers

VPL: Mtibwa Vs Yanga, Uwanja wa Jamhuri Morogoro

0

YANGA MTIBWA (2)Kikosi cha timu ya Yanga kinachomenyana na Mtibwa sugar, Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.YANGA MTIBWA (3)Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar.YANGA MTIBWA (4) YANGA MTIBWA (5)Donald Ngoma wa Yanga akichuana na mabeki wa Mtibwa.YANGA MTIBWA (6) YANGA MTIBWA (7)Malimi Busungu akinyang’anywa mpira na wachezaji wa Mtibwa Sugar.YANGA MTIBWA (8) YANGA MTIBWA (9) YANGA MTIBWA (10) YANGA MTIBWA (11) Ngoma na mpira wa kichwa.YANGA MTIBWA (12)Amiss Tambwe, Nadir Haroub Cannavaro wakipambana na Wanamtibwa.YANGA MTIBWA (13) YANGA MTIBWA (14) YANGA MTIBWA (15) YANGA MTIBWA (16)Vuta nikuvute.
YANGA MTIBWA (1)Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akisalimiana na mwandishi wa habari.

Dakika 90 zimekwisha, Yanga wanaondoka na pointi tatu mhimu baada ya kuilaza Mtibwa kwa bao 2-0 Uwanja wa Jmhuri mjini Morogoro. Yanga wanaendelea kujiklita kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa kuwa na pointi 15 baada ya kushinda mechi zao tano zote ambazo wamekwishacheza mpaka sasa.

GOOOOOOOOO Dk 89 Donald Ngoma anaifungia Yanga bao la pili baada ya kumalizia mpira aliotema kipa wa Mtibwa, Said Mohamed.

GOOOOOOOOO Dk 52 Malimi Busungu anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya mabeki wa Mtibwa Sugar kujichanganya na kipa wao wakati wakiwgombea mpira na Donald Ngoma

Dk 48, kona safi ndani ya lango la Mtibwa lakini Saidi Mohammed anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 47, Yanga wanapata faulo, Kamusoko anapiga shuti safi lakini linaokolewa na kuwa kona
MAPUMZIKO
KADI Dk 45+1 Telela naye analambwa kadi ya njano na mwamuzi ambaye aliamua kuzigawa sasa kama njugu
KADI Dk 45, Amissi Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi

Dk 40 hadi 44, bado inaonekana hakuna mashambulizi makali katika milando yote

KADI Dk 38, Salim Mbonde analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Busungu.

Dk 28 hadi 35, timu zinaonekana kucheza katikati zaidi kama bado kama vile zinasomana, kila upande uko makini katika upande wa safu ya ulinzi. Kwa Yanga ikiongozwa na Thabani Kamusoko na Mtibwa ni Shabani Nditi

Dk 27, Haji Mwinyi anaachia shuti lakini Said Mohammed anaokoa vizuri na kuwa kona
Dk 26, Kamusoko anachonga faulo nzuri lakini Mtibwa waokoa na kuwa kona ambayo ni ya tatu kwao, lakini haina mashara

Dk 24, Msuva anapiga kichwa safi baada ya Mtibwa Sugar kupata kona lakini Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 19, Ngoma anawatoka mabeki wawili wa Mtibwa Sugar lakini mpira unaokolewa na kuwa kona, hata hivyo haina mafanikio

Dk 15, Rajab anawatoka mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali, lakini mpira unapaa juu

KADI Dk 10 Selemani Rajab analambwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Cannavaro

Dk 4& 8, mpira zakdi unachezwa katikati ya uwanja, bado hakuna shambulizi kali kutoka kila upande. Ingawa Mtibwa Sugar wanaonekana kujipanga zaidi katika kiungo

Dk 2, Mtibwa Sujgar wanafika katika lango la Yanga, Yanga nao wanajibu na kuoata kona lakini haina madhara
Dk 1, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mtibwa, lakini si kwa shambulizi kali.

PICHA NA MUSSA MATEJA/GPL ALIYEKO MOROGORO

Leave A Reply