The House of Favourite Newspapers

LULU AUZA NGUO ZAKE KUSAIDIA WASIYOJIWEZA

STAA wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo Jumamosi, Januari 26, 2019 amewakabidhi nguo zake watu walionunua katika zoezi lake la kuuza baadhi ya nguo zake kwaajili ya kukusanya fedha ili kuwezesha project yake ya Save My Valentine, alilolenga kuwasaidia watu wasiojiweza.

Akizungumza wakati wa kukabishi nguo hizo, Lulu amesema kwa leo amekabidhi takribani nguo 36 kati ya 40 ambazo tayari zilikuwa zimeshapata wateja na kwamba mwitikio wa zoezi hilo umekua mzuri na unatia moyo kwa sababu watu wamepokea wazo lake vizuri na kumsapoti.

“Mimi nina nguo nyingi sana, hivyo nilifikiria baadhi ya nguo kuzigawa bure kwa watu wasiyojiweza, lakini zipo nilizokuwa nikenda nazo kwenye events na shoo, nikaja na wazo baada ya kuona bora niziuze ili nipate pesa ya kuwasaidia watu wasiyojiweza ambao kwangu mimi nitasherehekea nao Siku ya Wapendandanao kama Valentine wangu, Februari 14.

 

“Zoezi bado linaendelea, nitaposti tena jumatatu na watu wanaohitaji tutawasiliana ili wanunue. Ninafanya hivi kwa sababu nataka siku moja nikiondoka duniani niache alama ya mazuri niliyofanya, nimefanya mabaya mengi, nimepitia magumu mengi katika maisha yangu, lakini sasa hivi ni wakati wa kufanya angalau mema ili siku moja nikumbukwe kwa hiki ninachiokifanya,” alisema Lulu.

Na Edwin Lindege | GPL

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.