The House of Favourite Newspapers

Fatuma: Nina Maboifrendi Kibao

Fatuma Mustapha

SERENGETI Lite wameinoge­sha Ligi Kuu ya Wanawake ambayo msimu huu im­ekuwa na mengi ya kuvutia. JKT Queens ndiye bingwa mtetezi wa ligi hiyo, anazidi kuonyesha kuwa alistahili kuwa bingwa kutokana na uwezo mkubwa alionye­sha mpaka hivi sasa miongoni mwa timu zote 12 zinazoshiriki.

 

Imecheza michezo nane na kushinda yote,ina pointi 24. Imeweka rekodi ya kushinda ma­bao 16-0 kwenye mchezo mmoja.

Nyuma ya mafanikio hayo yupo Straika wao tegemeo Fatuma Mustapha ambaye mpaka sasa ame­shatumbukia kam­bani mara 17.

 

Ikumbukwe msimu uliopita Fatuma aliibuka mfungaji bora wa ligi hiyo baada ya kufunga mabao 18.

Amebakiza bao moja pekee ili kufikia reko­di yake ya mwaka jana na en­dapo atafani­kiwa kufunga bao kwenye mchezo wa leo dhidi ya Marsh Quuens ya Mwanza,atakuwa amevunja rekodi yake na kuanza safari ya kutengene­za ufalme mwingine kunako ligi hiyo.

 

Spoti Xtra limepata nafasi ya kuzungumza naye na hapa anaanza kufunguka mambo kadhaa.

“Kwa sasa nina miaka 22 na ninacheza ligi kuu ya wanawake zaidi ya msimu wa tatu,nimekuwa nikiinjoi zaidi kucheza mpira wa miguu kwa sababu ni moja ya vitu ambavyo navipenda sana.

NANI ALIKUSHAWI­SHI KUCHEZA SOKA?

“Hakuna aliyenishawishi kucheza soka ni kipaji tu ambacho mungu alinipa na ndiyo hivi tena mpaka leo nipo hapa.

 

KATIKA FAMILIA YENU WATU WAN­GAPI WANACHEZA SOKA?

“Kama wote hivi, isipokuwa dada yangu mkubwa yeye anacheza mchezo mwingine tofauti na mpira wa miguu, kwetu tumezaliwa watano wanne tu.

NANI ANAKUPA SAPO­TI KWENYE MAI­SHA YAKO YA SOKA?

“Familia yangu ni watu wa kwanza ambao siku zote huwa wananipa moyo na kunisisitiza nipam­banie kile ambacho nakiamini.

 

“Kitu kingine ni walimu wangu walionifundisha toka naanza soka la utotoni mpaka hapa nilipofikia leo ni watu ambao wamenisaidia kwa kiasi kikubwa.

 

ULIANZIA WAPI KUCHEZA SOKA?

“Nilianzia mtaani kwetu Urafiki Manzese,kwenye timu ya Future FC ambayo ipo mtaani kwetu kabisa,kisha nikajiunga na Sayari FC, Mbura­hati FC na leo nipo JKT Queens.

 

UMEFUNGA MA­BAO 17 KWENYE MECHI SITA NINI SIRI YA MAFANI­KIO?

“Kujituma na kumsikiliza mwalimu pamoja na kuwa na ushirikiano mkubwa na wache­zaji wenzangu hicho ndiyo kitu kinachonipa mafanikio.

 

TIMU GANI NYINGINE AMBAYO UNATAMANI KUCHEZEA?

‘’Kwa hapa nyumbani hakuna kwa sababu muda siyo mrefu nitakuwa kamanda hivyo sid­hani kama inaweza kuwa rahisi mimi kuchezea timu nyingine zaidi ya JKT Queens labda ije timu kutoka Ulaya naweza nikaangalia kama tunaweza kukubaliana.

 

MCHEZAJI GANI MWINGINE ANAKUPA CHANGAMOTO KWENYE LIGI YENU?

“Hakuna mchezaji ambaye ananipa changa­moto kwa sababu mimi najiamini na nina uamini uwezo wangu.

 

CHANGAMOTO ZIPI MNAKUTANA NAZO KWENYE LIGI?

“Wadhamini ndiyo changamoto kubwa sana kwenye soka la wanawake, kwa sababu utakuta timu inakosa hadi chakula, wakati mwingine inapata ugumu wa kusafiri kwenda kucheza ugenini mfano nje ya mkoa na sehemu zingine ambazo inalaz­imika kusafiri.

 

KWANINI WACHEZAJI WENGI HUJI­WEKA KAMA WANAUME?

“Muonekano tu na mtu anavyopendelea kuvaa,mbona kuna ambao wanacheza soka na wanavaa sketi mi nafikiri ni mtazamo tu wa watu.

 

VIPI KUHUSU KUWA NA MAHUSIA­NO YA JINSIA MOJA KWENYE TIMU ZA WANAWAKE?

“Siyo kweli nayo ni maneno tu ya watu, mimi binafsi yangu sijawahi kukutana na mambo kama hayo kwa muda wote niliocheza soka ila inawezekana yakawepo kwa jamii ny­ingine tofauti na hii ambayo naishi mimi.

 

UNATAMANI KUOLEWA?

“Ndiyo, lakini kwa mbeleni huko lazima nitakuwa na familia yangu pamoja na watoto ila siyo kwa sasa hivi muda bado wa kufanya hivyo.

 

UNABOYFRIEND?

“Ndiyo,tena ninao wengi tu!

 

MIPANGO YAKO MSIMU HUU IPOJE?

“Kuchukua tena ubingwa na kuwa mfungaji bora kwa mara ya pili mfululizo hayo diyo malengo ambayo nimejiwekea lakini kubwa zaidi nataka nifunge mabao mengi zaidi ya msimu uliopita na kujiwekea historia ambayo itakuwa ngumu kufikiwa na mtu yoyote.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.