The House of Favourite Newspapers

JUVENTUS YA RONALDO YAPIGWA 3-0

MABINGWA mara nne wa Kombe la Italia, Juventus, usiku wa kuamkia jana walijikuta wakipoteza mchezo na kuondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 3-0 na Atalanta.

 

Licha ya kumuanzisha staa wao katika mchezo huo wa robo fainali, Cristiano Ronaldo bado Juventus ilishindwa kufurukuta na kujikuta ikipoteza mchezo huo baada ya kufungwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza kabla ya kumalizia moja dakika za majeruhi.

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Atalanta kuifunga Juventus, mara ya mwisho kuifunga Juventus ilikuwa mwaka 2004 mabao 2-0 katika Kombe la Italia, tangu hapo ilipata sare tano na kufungwa mechi 21.

 

Kutokana na matokeo hayo, sasa Fiorentina itacheza nusu fainali dhidi ya Atalanta huku AC Milan wakitarajiwa kukutana na mshindi wa mchezo ulotarajiwa kupigwa usiku wa kuamkia leo, Inter Milan au Lazio.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.