CAF Yawazuia Simba Kuwachezesha Saa 8 Mchana

Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji.

SIMBA walitamani mechi yao dhidi ya Al Ahly ichezwe saa nane mchana kwenye jua kali lakini Caf imewapiga ‘stop’.

 

Ahly wanapokuwa nyumbani dhidi ya timu za Afrika Mashariki, hupanga mechi zao usiku wenye baridi kali ili kuwa katika mazingira mazuri ya kumvuruga mpinzani na kupata matokeo kirahisi.

 

Hivyo mashabiki wengi wa Simba, walitamani mechi dhidi ya Ahly ichezwe saa 8 mchana Jumanne kwenye jua kali ili walipize kisasi lakini uongozi umejibu haiwezekani.

 

Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji alisema kwamba; “Najua mnamaanisha nini, lakini kwa sasa haiwezekani, huwa kuna muda maalum ambao unapangwa kabla mashindano hayajaanza na mnakubaliana.”

 

“Kwa hiyo Caf wanaelekeza mechi zianze saa 10 kwa muda wa hapa, kinachoweza kufanyika ni kusogeza mbele muda ule lakini huwezi kurudisha nyuma ucheze saa 8,” alisema MO huku akicheka na kusisitiza kwamba anajua nia ya Wanasimba wengi.

 

Simba walitamani kuwachezesha Ahly kwenye jua kali la saa 8 kwa vile hali ya hewa ya Misri ni baridi na hakuna joto kali kama la Dar es Salaam.

Toa comment