The House of Favourite Newspapers

Simba vs Yanga …Mechi Ya Namba Jumamosi Taifa

Kikosi cha timu ya Simba.

KWA tathmini isiyo rasmi Watanzania wamejigawa kwenye timu mbili, Simba na Yanga. Hizo ndizo timu za mashabiki wengi hapa nchini, ni nadra sana kukuta mtu hazishangilii timu hizo pacha.

 

Ushahidi huo unaonyesha pale ambapo wanapokutana uwanja hujaa na kupambwa na rangi mbili ile ya kijani na nyekundu. Jumamosi hii timu hizo zitakutana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

 

Huu ni mchezo wa pili kwao kukutana kwa msimu huu baada ya ule wa awali uliopigwa mwaka jana na kumalizika kwa suluhu. Mechi hii imekusanya mambo mengi lakini makala haya yanakuchambulia mechi hii kwa namba.
Namba 102


Hii ni namba ambayo inasimama ikimaanisha timu hizi tangu zilipoanza kukutana kwa kipindi hicho hadi Jumamosi utakuwa mchezo wa 102 kwa timu zote mbili, hii ni kweli ligi kuu pekee.

Rekodi zinaonyesha Yanga ndiyo wamekuwa wababe katika mechi hizi za dabi wakishinda 36 Simba wameshinda 27 na sare 35.

 

Namba 22
Namba hii inasimama nyuma ya pointi ambazo Yanga wamewaacha watani zao Simba kwenye msimamo wa ligi kuu hadi sasa.
Yanga ndiyo vinara wakiwa na pointi 58 huku Simba wakiwa na pointi 36. Yanga wapo mbele kwa mechi nane dhidi ya Simba.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Namba 7
Hii inasimama ikiwakilisha wachezaji waliocheza klabu zote mbili za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti kwenye mechi hii.
Nyota ambao wamekipiga klabu zote hizo ni Deogratius Munishi, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima kwa Simba wakati Yanga wakiwa na Haruna Moshi ‘Boban’, Kelvin Yondani, Amissi Tambwe na Ibrahim Ajibu.

 

Namba 16
Hii ni inasimama siku husika wakati timu hizi mbili zinaopokutana yaani Februari 16. Hii ni mechi ya saba kwao kukutana ndani ya mwezi Februari.

Namba 2
Makocha Mwinyi Zahera wa Yanga na Patrick Aussems wa Simba, ni mara yao ya pili kukutana tangu waanze kuvifundisha vikosi hivyo.
Mara ya kwanza walipokutana makocha hawa hakuna aliyeibuka mbabe wa mwenzake.

 

Namba 11
Heritier Makambo wa Yanga ndiye anasimama kama mchezaji mwenye mabao mengi wakati wa mechi hii baada ya kutupia kambani mabao 11.
Hakuna mchezaji mwenye mabao mengi kuliko yeye miongoni mwa wale wa Yanga na Simba. Meddie Kagere wa Simba ndiye anamfuata Makambo kwa mbali baada ya kufunga mabao nane.

 

Namba 0
Katika pambano lililopita lililopigwa Novemba 30, mwaka jana baina ya timu hizi lilimalizika kwa suluhu yaani 0-0. Hakukuwa na timu yoyote ile ambayo ilifunga bao kwa mpinzani wake.

 

Namba 1
Kwenye pambano hili Yanga wanaingia wakiwa wakiwa ndiyo vinara wa ligi wakiwa na pointi zao 58 baada ya mechi 23. Simba wao wapo nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya pointi 36.

 

Namba 8
Hii ni idadi ya wachezaji ambao watakosekana kwenye mechi hii ya pili licha ya kuwepo kwenye mechi ile ya kwanza. Wachezaji ambao watakosekana kwa Simba ni Shiza Kichuya (kauzwa Misri), Marcel Kaheza (yupo Kenya), Mohammed Rashid (yupo KMC kwa mkopo) na Shomary Kapombe (majeruhi).
Kwa upande wa Yanga watawakosa Beno Kakolanya (hayupo katika timu), Yusuph Mhilu na Pato Ngonyani wote wapo mkopo na kinda Yohana Nkomola.

Comments are closed.