The House of Favourite Newspapers

Dully Sykes aikataa adhabu ya Nyoso

0

Juma-NyossoMSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, amesema anaamini adhabu aliyopewa beki Juma Nyosso ya kutocheza miaka miwili ni uonevu.

Dully ambaye anajulikana na nyimbo zake kibao kama Salome na Julietha, alizotamba nazo enzi zake, alisema Nyosso amekosea, hasa kurudia mara ya pili, lakini adhabu hiyo imekwenda kisiasa na kulenga kumkomoa.

“Sikiliza ndugu, mnapopambana kila mchezaji anafanya ujanja kuwachanganya wapinzani. Ikiwezekana anataka kumtengenezea kadi nyekundu mchezaji wa timu pinzani.

“Si umeona Chelsea kuna kina Diego Costa. Italia Mario Balotelli, pia unamkumbuka Gazza (Paul Gascoigne) wa England? Wote hao ni vichaa wa soka.

“Hata katika muziki tuna akina Balotelli, mfano mimi hapa. Pia kuna wachezaji wapole na wasanii wastaarabu kama akina AY, MwanaFA. Yote haya yapo.

“Nafikiri kama ni adhabu kutokana na makosa yake, basi wangempa adhabu ya miezi sita angalau, lakini siyo miaka miwili. Unajua wanataka kufanya alichofanya kionekane kitu cha ajabu sana katika soka. Wakati ni mambo yanayoendelea kila siku.

“Mimi nilikuwa kipa wakati nacheza soka, Nyosso ni beki wangu, nimekua naye pamoja kule Ilala. Hakuwa mtu wa namna hiyo, lakini najua alikuwa anapambana kwa ajili ya timu yake,” alisema Dully.

Tayari Nyosso ameanza kutumikia adhabu hiyo ikiwa ni ya pili baada ya ile ya kufungiwa mechi nane baada ya kumtomasa Elius Maguli wakati akiwa Simba, Januari, mwaka huu.

Leave A Reply