Kipenga cha Uchaguzi Chapigwa Nigeria

 

WANIGERIA leo wanashiriki uchaguzi mkuu baada ya shughuli hiyo kuahirishwa ghafla wiki moja iliyopita.

 

Wagombea wawili wakuu ni Rais Muhammadu Buhari, 76, na naibu wa rais wa zamani Atiku Abubakar, 72.

 

Buhari anasema amejenga msingi thabiti wa ustawi wa jamii lakini mpinzani wake anadai miundo mbinu ya utawala haifanyi kazi Nigeria.

 

Yeyote atakayeshinda uchaguzi huu anakabiliwa na kibarua cha kushughulikia masuala ya uhaba wa umeme, ufisadi, tishio la usalama na mdororo wa uchumi.

 

Haijabinika matokeo ya uchaguzi yatatolewa lini, huenda ikawa Jumatatu, Jumanne, ama baadaye.

 

Uchaguzi wa awali ulikuwa umepangiwa kufanyika Jumamosi ya Februari 16 mwaka huu lakini tume huru ya uchaguzi (Inec) ikatangaza kuahirishwa kwa shughuli hiyo saa tano kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.

 

Tume hiyo imetoa sababu kadhaa ya kuchelewesha uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na jaribio la kuhujumu shughuli hiyo, changamoto za kiufundi na hali mbaya ya hewa.

 

Inec, hata hivyo, imethibitisha kuwa mara hii iko tayari kuendesha uchaguzi huo.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment