The House of Favourite Newspapers

WEMA NIMEKAA MIEZI SITA BILA KUFANYA MAPENZI

Wema Isaac Sepetu.

UNAPOTAJA majina ya wanyange bora ambao wame­dumu kwa zaidi ya miaka 10 wakiwa juu basi huwezi kumuweka kando Wema Isaac Sepetu.

 

Wema ambaye mashabiki zake wan­amtambua zaidi kama Madame, ustaa wake umekuwa na mambo na vituko vingi vya hapa na pale.

 

Ukianza kuhesabu msururu wa wa­naume aliotoka nao, ni mrefu mno, lakini hivi sasa anasema hana mtu tangu Sep­temba, mwaka jana.

 

Hivi karibuni katika Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) alifanya mahojiano na vyombo vya habari na kujibu maswali mbalimbali kama ifuatavyo.


UNA NYWELE FUPI KWA SASA, JE UTABADILISHA?

“Huu ni mwonekano ambao nimeamua kuwa nao kwa mwaka 2019 mzima, sitabadilisha.

“Labda mkiniona kwenye kazi ndiyo naweza ku­badilika lakini hivi mkin­iona mimi sitabadilika.

“Ninasikia raha sababu Dar kuna joto.

 

VIPI MAHUSIANO?

“Niko ‘single’ tangu mwezi wa tisa mwaka jana, tena sija-du na mtu yeyote.

 

KUNA WANAUME WA­NAOKUFUATA?

“Wako wengi sana, yaani wengimno, mpaka daaah!

 

UNAWEZAJE KUKAA SIN­GLE KWA MUDA WOTE HUO?

“Kuna muda mtu unaona bora upumzike masuala hayo, kama mimi nimechukua muda wa kuwa mwenyewe tu bila ya masuala hayo.

 

 

“Ninaweza kujizuia, tena watu ambao wanaonizunguka na kunipenda wananipa furaha.

 

ULISEMA HUIPENDI INSTA­GRAM, KWA NINI?

“Siyo kama siipendi Insta ila sipendi mambo yake ya huko, yaani kama mambo ya umbea. Ninachofanya ninaitumia kama sehemu ya kutangaza biashara zangu.

“Tena kama nikiposti kitu sitaki kuanga­lia komenti, naenda WhatsApp, ninatafuta vitu vya kunifanya niwe bize. Sipendi um­bea.

 

KWA NINI UNAPENDA KUVAA MAVAZI MEUSI?

“Kwa sababu mavazi haya hayajawahi kumuangusha mtu, kwenye ‘event’ kama hizi huwezi tu kujivalia lazima uvae kama hivi.

VIPI MASULA YA KUWA NA MTOTO?

“Mwenyezi Mun­gu akinibariki nita­mshukuru, nitase­ma Alhamdulillah.

 

NINI MI­PANGO YA WEMA MWAKA HUU?

“Watu wasubiri kuona kitu gani nitafanya, nina vitu vingi sana kwa mwaka huu lakini siwezi ku­visema kwa sasa.

 

MWAKA JANA NA HUU KWAKO KUNA TOFAUTI GANI KWENYE FILAMU?

“Nimekaza tu pa­lepale, kila siku nime­kuwa nikisema nataka kuwa zaidi ya jana. Una­jua naipenda kazi nisiwe muongo naichukulia sana siriazi, nadhani ni hivyo,” anasema Wema.

Makala – Bongo | SAID ALLY

Comments are closed.