Mkataba Wa Ajibu Wazuiwa Yanga

HATA atupie mabao matamu kiasi gani, mkataba wa nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajibu hautaguswa wala kuongezwa mpaka msimu umalizike.

 

Ajibu amekuwa akihusishwa kurejea Simba kutokana na mabosi wake wa zamani kukubali uwezo wake licha ya kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems kusonya kusema ni wa kawaida sana.

 

Meneja wa Ajibu ambaye ni ndugu yake, Athuman Ajibu amesema kuwa kwa sasa anasubiri mkataba umalizike ndipo atajua ampeleke wapi mteja wake kwani ofa alizopata zinampa nguvu ya kuamua nini afanye.

 

“Ajibu mkataba wake unamalizika msimu unapoisha nimeamua kutoruhusu kuongezea mkataba wake ili kuona ni timu ipi ambayo itamfaa kutokana na ofa ambazo zipo mkononi kwa sasa.

 

“Kwa sasa bado ni mali ya Yanga na kuna timu ambazo tumekuwa tukifanya nazo mawasiliano ila siwezi kuweka wazi kwa sasa, uongozi wa Yanga unajua na nimewaambia wazi kwamba inabidi tusubiri kabla ya kuongeza mkataba kwenye timu yake,” alisema.

 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussen Nyika alipotafutwa azungumzie suala hili alisema kuwa yupo kwenye kikao.

Ajibu kwa sasa ni kinara wa assist bongo ambapo kwa sasa anazo 15 huku akitupia pia mabao 6 ligi kuu Bara.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Toa comment