JKT Queens Kiboko, Yapania Kubeba Kombe Lao

TIMU ya JKT Queens imedhihirisha kwamba ni moto wa kuotea mbali baada ya kucheza michezo 14 bila kupoteza hata mmoja huku uongozi ukisisitiza unahitaji kutetea kombe lao.
JKT Queens ambao wanashiriki ligi ya wanawake inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Lite ni vinara kwa sasa kwenye ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 42.
Akizungumza na Championi Jumatano, kocha mkuu, Ally Ally, alisema kuwa uzoefu wa ligi pamoja na wachezaji kujituma unawapa matokeo chanya kwenye michezo yao wanayocheza.
“Ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa ila kinachonisaidia ni uzoefu pamoja na juhudi za wachezaji uwanjani, hali hii inanipa matumaini ya kutetea kombe letu msimu huu.
“Hakuna kitu chepesi kwani kila timu ambayo tunacheza nayo inakaza ili kuvunja rekodi ila inakwama kutokana na maandalizi na mbinu ambazo ninawapa wachezaji wangu kila siku, tuna mabao 82, tumefungwa matatu pekee,” alisema Ally.


Comments are closed.