Wasomaji Wasema: Betika Linarahisisha Kazi Yetu ya Kubeti
WASOMAJI wa gazeti la Betika katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam yakiwemo Gongo la Mboto, Ukonga na Mombasa, wamelisifia gazeti hilo na kusema kwamba linarahisisha kazi yao ya kubeti.
Betika ambalo lina kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, linaingia mtaani kila Jumatano likiwa na makala na odds za kampuni mbalimbali pamoja na takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.
Leo Alhamisi, wasomaji waliofikiwa na timu ya maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, walisema hivi sasa wanapotaka kubeti, hawatumii muda mwingi kuweka mkeka, kwani kwa kupitia Betika wanaifanya kazi hiyo kwa muda mfupi sana.
“Zamani nilikuwa natumia muda mwingi sana kukaa na kuanza kuzichambua timu kabla ya kubeti, lakini hivi sasa natumia muda mchache kwa sababu huwa nalitumia gazeti la Betika katika kazi hiyo.
“Betika linarahisisha sana kazi yetu hii kwa sababu lina kila kitu ambacho tunakihitaji kwenye kubeti, kikubwa nawashauri wengine wanaobeti kama mimi walitumie gazeti hili kufanikisha ushindi wanapobeti,” alisema mmoja wa wasomaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Issa.
Kwa upande wa Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kiu yao kubwa ni kuhakikisha wasomaji wanaendelea kuliamini gazeti hilo katika masuala yote ya kubeti kama ambavyo malengo yao yalivyo.
“Malengo yetu tangu tunalianzisha gazeti hili ni kuhakikisha tunarahisisha kazi ya wale jamaa wa kubeti na kwa kuthibitisha hilo, kila siku tumekuwa tukipokea maoni na pongezi mbalimbali ambazo tumekuwa tukitumia kulifanyia maboresho zaidi gazeti hili,” alisema Mgema.
Mgema aliongeza kuwa, bado nafasi zipo wazi kwa wale ambao wanahitaji kutangaza na gazeti hilo ambapo wanatakiwa kufika zilipo ofisi zao Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
PICHA NA DENIS MTIMA | GPL
Comments are closed.