Mazembe wataka mashabiki wao wawaige Simba

KITENDO cha kishujaa kilichofanywa na shabiki wa Simba kutoka Mbeya mpaka Dar es Salaam kuja kutazama mechi dhidi ya TP Mazembe, kimewakosha Wakongo hao.

 

Wakongo hao wameshangazwa na ushujaa uliofanywa na Ramadhani Mohammed na wamemposti kwenye mitandao yao baada ya kurudi Lubumbashi mechi hiyo ikimalizika kwa suluhu.

Katika mtandao wao wa klabu, walimposti shabiki huyo na kuwataka Mazembe wataka mashabiki wao wawaige Simba mashabiki wao kuiga kitendo hicho cha kilichoonyesha mapenzi ya kupitiliza kwa timu yake. Mazembe wamewasihi mashabiki wao ambao wataweza kufanya mambo ya kukumbukwa kama hayo wayatume ili klabu ijue na kujivunia kama alivyofanya mwenzao wa Simba.

Simba na Mazembe wanarudiana keshokutwa Jumamosi jijini Lubumbashi huku uongozi wa Wakongo hao ukiwasisitiza mashabiki kujazana uwanjani kwa vile mechi hiyo ni muhimu. Simba wanahitaji sare yoyote ya mabao kusonga mbele hatua ya nusu fainali ambayo ina fedha za kufa mtu.


Loading...

Toa comment