The House of Favourite Newspapers

Simba na JKT Queens ni kisasi

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inayodhaminiwa na Bia laini ya SERENGETI LITE inaendelea tena leo ambapo JKT Queens watavaana na Simba Queens katika uwanja wa Isamuhyo, Mbweni.

 

Mechi hii ni ya mzunguko wa pili katika ligi hiyo ya Wanawake ambapo katika mzunguko wa kwanza, Simba ilipoteza kwa kichapo cha bao 1-0, katika uwanja wa Karume Ilala Jijini Dar.

Akizugumza na Spoti Xtra, Kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi alisema kuwa hawatakubali kupoteza kwa mara ya pili.

 

“Hatutakubali kupoteza,ingawa tunaenda kucheza na timu bora ambayo nadhani itatupa kipimo halisi kwamba tumefika wapi na tunatakiwa tufanye nini,hivyo ushindi ni muhimu zaidi,’’alisema Mgosi ambaye ni mchezaji wa zamani wa DC Motema Pembe, Simba na Mtibwa.

 

Ikumbukwe JKT Queens ni timu pekee ambayo mpaka sasa haijapoteza mechi hata moja.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Comments are closed.