The House of Favourite Newspapers

Kocha msomi arejeshwa Simba

Kocha msaidizi wa Simba, Denis Kitambi (kushoto).

WAKATI wowote Kocha msaidizi wa Simba, Denis Kitambi atarejea kwenye benchi la ufundi la Simba na atakuwepo katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania. Kitambi ndiye Kocha mzawa msomi zaidi kwa sasa kwani ana leseni B ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA).

 

Habari zinasema kwamba alijiondoa kwenye benchi baada ya kutopewa mkataba na barua ya uthibitisho wa kazi katika miezi yake minne ndani ya klabu hiyo.

 

“Kilichotokea ni yeye kutaka mkataba na nakala yake uthibitisho wa kazi yake kwa sababu mshahara na posho zote anapata kwa wakati isipokuwa ni hilo la mkataba na nakala ya kuthibitisha kwamba ni muajiriwa wa Simba hivyo sasa atakuwepo kwenye mechi na JKT maana anajindaa kutoka kwao Morogoro kuja Dar,” alithibitisha mmoja wa vigogo wa Simba jana mjini Musoma kwamba wameshamalizana.

 

Spoti Xtra linajua Kitambi yupo Jijini Dar es Salaam lakini jana alipoulizwa kuhusu ishu yake hakutaka kuzungumza lolote.

Comments are closed.