The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Masele aripoti bungeni Jumatatu saa 5, akikaidi atakamatwa

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele anatakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kesho Jumatatu kabla ya saa tano asubuhi.

 

Akizungumza  jana Ndugai alisema ikiwa mbunge huyo hatofika ndani ya muda huo litatolewa agizo la kumkamata na kumfikisha katika kamati hiyo.

 

Masele ameibua sintofahamu baada ya kutuhumiwa kugonganisha mihimili ya nchi na kwa kile ambacho Ndugai alikiita kufanya mambo ya hovyohovyo, hivyo kuitwa arejee nyumbani na Spika huyo kutoka Afrika Kusini alikokuwa anahudhuria vikao vya Bunge la Afrika (PAP).

“Mwisho Jumatatu, saa tano asubuhi awe ameshafika na ikiwa hajafika itatolewa hati ya kukamatwa kwa sasa bado ni mtu wa kawaida,” alisema Ndugai.

 

Alipoulizwa kama ana uwezo wa kumtaka Masele kurejea nchini na kuandika barua kwa PAP kusimamisha kwa muda ubunge hadi itakapotolewa taarifa nyingine, Ndugai alisema, “Unapokuwa mwakilishi wetu sisi ndio tumekupeleka, si wale (PAP) ndio wamekuchukua huku.” Aliongeza, “anayesaini barua ya kwenda huko ni nani…, Spika sasa kama ni hivyo kwa nini nishindwe kukurudisha. Yaani rais umteue waziri halafu ushindwe kumtengua. Tulimtaka arudi anapaswa kurudi.”

 

Ndugai alisema uwezo ambao hana kwa Masele ni kumfukuza ubunge wake wa Shinyanga Mjini. “Alichaguliwa na wabunge ndani ya Bunge lakini kumsimamisha na kumrudisha anatakiwa katika mahakama ya Bunge uwezo huo ninao, lengo ni atoke huko arudi ni lazima tusimamishe unachokifanya ili lengo urudi. Anasahau kuwa anawakilisha nyumbani, wakikuita nyumbani lazima uende,” alisema.

Habari na Fidelis Butahe, Mwananchi

Comments are closed.