Usipime Simba vs Sevilla leo Taifa ni Shoo ya Kibingwa

SIMBA wamewaahidi mashabiki wao shoo ya kibingwa leo Alhamisi usiku kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Sevilla ya Hispania. Lakini Wapinzani wao wamewacheki weee…wakasema “tukutane uwanjani.”

 

Kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussem ameuahidi uongozi na mashabiki kutandazia soka safi lenye hadhi ya mabingwa wa nchi.

Simba wataingia uwanjani hapo wakiwa tayari wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara baada ya juzi kuwafunga Singida United na kujihakikishia ubingwa huo na nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwezi Agosti.

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Cresentius Magori alisema kuwa juzi usiku alikutana na kocha huyo baada ya mchezo wa Singida na kuzungumza naye na amemuahidi kupanga kikosi imara cha ushindi huku wakionyesha kiwango kikubwa.

 

Aliongeza kuwa, wanataka kupata ushindi katika mchezo kwa lengo la kuchukua kikombe kikichowekwa ili waweke rekodi ya kuchukua kikombe cha pili mfululizo baada kile cha ligi ambacho Yanga na Azam wameambulia patupu.

“Tunafahamu umuhimu mkubwa wa mchezo huu wa kirafiki wa kimataifa, hivyo ni lazima tushinde ili tuweke historia.

 

“Mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kwa ajili ya kuisapoti timu yao,” alisema Magori ambaye ndiye kiongozi msomi zaidi kwenye ngazi klabu baada ya Mshindo Msolla ambaye ni Mwenyekiti wa Yanga.

Naye Rais wa Sevilla, Jose Ramon Carmona alisema kuwa: “Niwashukuru SportPesa kwa kufanikisha ujio wetu kwa kuwa klabu ya kwanza La Liga kufika hapa nchini Tanzania.

 

“Kuhusu maandalizi yapo vizuri ya mchezo huu, tumepata taarifa za Simba kuchukua ubingwa wa 20 jana (juzi), hivyo niwapongeze kwa hilo, hivyo tutaingia uwanjani kwa ajili ya kazi moja pekee ya ushindi.


Loading...

Toa comment