The House of Favourite Newspapers

BREAKING: WEMA KUKAMATWA KWA KUKIUKA DHAMANA

 

Wema  Sepetu.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata mwigizaji Wema  Sepetu kwa kosa la kuruka dhamana baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa mshtakiwa hyo hayuko Mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

 

Hati hiyo ya kumkamata imetolewa leo Juni 11 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonda, baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Silvia Mitanto kudai kwamba mshtakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote.

 

Wakili wa utetezi, Ruben Simwanza, amedai mshtakiwa alifika mahakamani lakini kaumwa hivyo ameshindwa kuingia katika chumba cha mahakama.

 

Akitoa uamuzi,  Hakimu Maira amesema mahakama inatoa hati ya kumkamata mshtakiwa kwa sababu kama alifika alishindwa nini kuingia mahakamani.

 

Mwigizaji huyo anakabiliwa na shtaka  la kuchapisha video ya ngono katika mtandao wa kijamii.

 

Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

Comments are closed.