2Face Asherehekea kugonga miaka 40
Mkongwe wa muziki kutoka Naija, Innocent Ujah Idibia ‘2 Face’
MKONGWE wa muziki kutoka Naija, Innocent Ujah Idibia ‘2 Face’ juzi kati alisherehekea kutimiza miaka 40 kwa kufanya bonge la pati pamoja na mastaa wenzake.
Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya kimataifa, Eko iliyopo pande za Victoria Island, Lagos ambapo 2 Face alikuwa ameambatana na mkewe, Annie nee Macaulay.
Miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni Basketmouth, Seyi Shay, Waje, Jeremiah Obodo, Alex Akubo na wengine kibao.