HARUSI YA BABU SEYA, SHANGWE KAMA LOTE (PICHA +VIDEO)

Mwanamuziki mkongwe, Nguza Viking ‘Babu Seya’ akiwa na mkewe, Bi Desderia Philip Haule wakifanya yao kwenye Ukumbi wa Hotel ya Landmark iliyopo Mbezi Beach.

SHAMRASHAMRA za harusi baada ya mwanamuziki mkongwe, Nguza Viking maarufu Babu Seya, zimefanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya jana Jumamosi kufunga ndoa na Bi.Esteria Haule katika Kanisa Takatifu Katoliki Parokia ya Bikira Maria, Sinza, Dar ambapo wageni waalikwa walifaidi vya kutosha.

Mikogo ya kulishana keki kimahaba.

Baba na mwana wakicheza na kuimba.

Muonekano ndani ya ukumbi.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo akiongoza mduara wakati mambo yakiwa yamekolea ukumbini hapo.

Baba wa Bi Harusi mwenye suti akiwa na kampani yake wakati wakienda kutunza.

Zawadi zikipelekwa kwa mbwembwe na madaha.

…Wakiendelea kutoa zawadi.

…Burudani ikiendelea.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL


Loading...

Toa comment