Mbelgiji Ampa Majukumu Mawili Sheva Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems ameonekana kunogewa na kiungo wake mshambuliaji, Miraji Athumani ‘Sheva’ kwa kumpa majukumu mawili kwenye kikosi hicho.

 

Sheva ni kati ya usajili bora uliofanywa na timu hiyo kwenye msimu huu baada ya kufanikiwa kufunga mabao matatu, akisababisha penalti mbili huku akipiga pasi safi ya bao moja.

 

Kiungo huyo ametengeneza rekodi hiyo nzuri akiwa na msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na Simba huku akiwaweka benchi mastaa kibao waliosajiliwa kwa mkwanja mrefu na kwa mipango ilivyo, Meddie Kagere ana nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Aussems alisema kuwa ana matarajio makubwa ya kiungo huyo kufanya vema kwenye msimu huu kutokana na mwanzo mzuri aliokuwa ndani ya klabu kubwa ya Simba.

 

Aussems alisema kuwa kiungo huyo anatakiwa kufanya majukumu mawili kwa wakati mmoja kwenye mechi ambayo amempa ili kuhakikisha anaipa timu ushindi.

 

Aliongeza kuwa majukumu hayo aliyompa kiungo huyo ni kuwatengenezea nafasi za kufunga mabao washambuliaji wa timu hiyo wakiongozwa na Kagere na John Bocco ambapo kama Kagere naye ataendelea na kasi aliyonayo sasa atakuwa na nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora msimu huu.

 

“Kiukweli nimevutiwa na kiwango kikubwa ambacho amekionyesha Miraji ndani ya muda mfupi tangu ajiunge na Simba.

“Ni mchezaji anayecheza kwa kujituma akiwa ndani ya uwanja, pia sifa yake nyingine kubwa ni kucheza kwa kufuata maelekezo yangu uwanjani.

 

“Nilikaa na kuzungumza naye hivi karibuni na kumtaka afanye majukumu mawili ndani ya wakati mmoja ambayo ni kutengeneza nafasi za kufunga mabao kwa washambuliaji ambayo ninaamini anaimudu, pia afunge mabao, tayari ameianza akifunga mabao matatu katika ligi,” alisema Aussems.

Stori Wilbert Molandi | Championi


Loading...

Toa comment