Sheikh Kishki Atembelea Ofisi za Global Group
MSIMAMIZI Mkuu wa Taasisi ya Al Hikma Foundation, Sheikh Nurdeen Kishki, leo Alhamisi Oktoba 17, 2019M amefanya ziara katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori Dar es salaam, kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Idara mbalimbali.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Global Radio baada ya ziara hiyo, Sheikh Kishki amesema kutokana na kazi zinazozalishwa na vituo pendwa vya Global Group amevutiwa kujifunza vinavyofanya kazi.
Aidha amekumbushia umuhimu wa kuzingatia maadili katika jamii na kuepuka vitendo viovu vikiwemo vya matumizi mabaya mitandao.
Pia ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura na kuwachagua viongozi wanaostahili kuwaongoza.
Comments are closed.