The House of Favourite Newspapers

Bobi Wine Ashitakiwa Akidaiwa Kudanganya Umri Wake

0

MAHAKAMA nchini Uganda imemtaka mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kufika mbele yake kujibu tuhuma za kutoa taarifa za uwongo kuhusu umri wake kwa Tume ya Uchaguzi.

 

Bobi Wine anatakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo kabla ya Septemba 16 kujibu kesi iliyowasilishwa na wakili, Male Mabirizi.

 

Katika ombi lake la Agosti 3,  Mabirizi anadai vyeti vya masomo vya Bobi Wine vinaonesha alizaliwa tarehe 12 Februari 1980, tofauti na tarehe iliyonakiliwa katika pasipoti yake na pamoja na fomu aliyowasilisha kwa tume ya uchaguzi mwaka 2017 wakati alipoteuliwa kugombea kiti cha ubunge.

 

Pasipoti ya Bobi Wine inaonyesha kuwa alizaliwa Februari 12, 1982. Pia, anakabiliwa na mashitaka ya “kupata usajili kwa njia ya udanganyifu” katika mahakama hiyo.

 

Mjadala kuhusu miaka ya mtia nia huyo wa kugombea kiti cha urais na uhalisia wa vyeti vyake vya elimu umezua gumzo katika mitandao ya kijamii kwa majuma kadhaa.

 

Bobi Wine aliweka ujumbe katika mtandao wa Facebook Siku ya Jumatatu, akisema kesi ya hivi punde dhidi yake ni sehemu ya mwendelezo wa njama za serikali kuhujumu upinzani akisema madai hayo ni jaribio lingine la kuhujumu upinzani.

Leave A Reply