Mr Blue na Mkewe Wapata Mtoto

MIONGONI mwa stori zilizotengeneza headlines kwenye social media ni kuhusu msanii Khery Sameer Rajab maarufu kama Mr Blue ambaye kupitia post yake ya Instagram ameeleza kuwa amepata mtoto mwingine na mkewe Waheeda.

 

“Ahsante mke wangu Mrs Blue Beauty Cosmetics kwa zawadi nyingine alhamdulillah, ahsante sana Mungu kwa kheri zako, karibu sana binti yangu Khairat kwenye familia alhamdulillah, Mungu ni mwema sana,” ameandika Mr Blue.

Huyo atakuwa mtoto wa tatu kwa msanii huyo na mkewe kwani hapo awali walikuwa na watoto wawili ambao mmoja ni wa kiume mwingine  wa kike.

Toa comment