The House of Favourite Newspapers

40 ya Tiffah yaacha Madeni!

0

TIFFAH DIAMOND (3)Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  na mpenzi wake Zari wakiwa na mtoto wao Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’.

https://www.youtube.com/watch?v=XP70rbMigMQ

OHOOO! Kuna madai kwamba, ile pati ya kukata na shoka ya kutimiza siku 40 kwa mtoto wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliisha huku nyuma ikiacha madeni ya kiasi cha shilingi 1,005,000, Amani limechimbua.

DIAMOND TIFFAH'S 40 (10)Diamond akiwa na Zarinah Hassan.

Ni siku ya 11 sasa, kampuni iliyopewa tenda ya kupamba kwenye shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa staa huyo, Tegeta-Madale, Dar ya Rachel Decorations imejipambanua kuwa, inamdai baba Tiffah kiasi hicho cha fedha na hakuna matumaini ya kulipwa.

DIAMOND TIFFAH'S 40 (3)

DIAMOND TIFFAH'S 40 (4)Wanafunzi wa Madrasa nao wapo kwa ajili ya 40 ya Tiffah. 

MENEJA WA KAMPUNI AZUNGUMZA

Akizungumza na Amani, meneja wa kampuni hiyo ya mapambo aliyejitaja kwa jina moja la Lutengano akisema linatosha, alisema wiki moja kabla ya sherehe hiyo iliyokuwa na mbwembewe nyingi, dada wa Diamond, Esma Platnumz alimtafuta mpambaji huyo na kumwambia kuwa, kuna tenda.

“Bosi wangu anaitwa Rachel, ndiye aliyekutana na Esma wakakubaliana kisha wakaenda kwa Diamond kwa ajili ya makubaliano ya kifedha lakini bajeti ilikataliwa baada ya kuonekana ndogo na baadaye wakaafikiana kwamba, afanye kazi kutokana na kiasi cha fedha alichoahidi.

tiffah Mtoto wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’.

DIAMOND AINGILIA KAZI ZA WATU

“Siku moja kabla ya tukio (Jumamosi), usiku tulikwenda nyumbani kwa Diamond (Madale) na vifaa vyetu kwa ajili ya kuanza kazi kwa kuwa shughuli ilitakiwa kufanyika asubuhi lakini tukiwa katika maandalizi ya kufunga matenti (turubali), Diamond aliingia na baadaye akatoka, akaanza kuelekeza anavyotaka kupambwe.

“Tulimweleza kwamba haiwezekani kutokana na fedha ndogo waliyokuwa wametoa, akaahidi kwamba yuko tayari kuongeza fedha ilimradi mapambo yaenee kama anavyotaka na kusema kuwa ana watu wa muhimu watakaofika hapo hivyo panatakiwa pawe na hadhi zao. Ikabidi tuanze kuchukua vipimo upya,” alisema meneja huyo.

DIAMOND TIFFAH'S 40 (8)Mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim, akirembwa.

MAKUBALIANO MAPYA

Lutengano aliendelea kuliambia Amani kuwa, ilibidi wakubaliane na Diamond upya, kwamba kama anataka kuongeza sehemu ya mapambo basi gharama ilibidi iongezeke, akakubaliana na vyote na kutoa fedha kiasi kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo huku akisema fedha iliyobaki angetoa siku ya sherehe huku akisema kuwa, mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alipendelea zaidi makapeti na mito siyo viti kama ilivyokuwa mwanzo.

“Tukawa tumekubaliana aongeze shilingi milioni 1,600,000 kwa sababu kulikuwa na vitu ambavyo vilitakiwa kununuliwa, Diamond alitoa shilingi  moilioni 1,300,000 na kubakisha shilingi laki 300,000 lakini pia kabla ya hapo alikuwa akidaiwa shilingi laki 625,000 kama fedha ya matenti 5 ambapo kila tenti liligharimu shilingi 125,000.

DIAMOND TIFFAH'S 40 (1)Maandalizi yakiwa yamepamba moto nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar.

“Baada ya matenti yote kufungwa, tukasitisha zoezi la mapambo kuendelea na mimi siku hiyo sikulala,  nikaanza kushughulikia makapeti ambayo Diamond aliagiza  mpaka nikaja kuyapata muda ulikuwa umeshakwenda na hilo tulishakubaliana kwamba kunaweza kutokea tukacheelewa kwa sababu ya muda kuwa mbaya akasema yeye anataka iwe hivyo alivyopanga.

Lutengano anasema baada ya kuzunguka sana Kariakoo, alifanikiwa kupata makapeti aliyoagizwa na kuyapakia kwenye gari la mizigo kisha kuagiza gari liende Madale huku yeye akiendelea kutafuta mito na maua.

“Kutokana na muda ulivyokuwa umekwenda gari lilifika Madale saa 3:00 asubuhi na wenyeji wakawa wamesusa kwamba vitu vimechelewa, vitu vikashushwa ikabidi tena mimi nianze kuwaelewesha kwa njia ya simu namna ambavyo tulikubaliana na Diamond mwenyewe na baadaye vitu vikaandaliwa na sherehe ikaanza.

“Kwa kuwa mimi nilikuwa nimechoka, ule muda ambao sasa mtoto ndiyo alikuwa anatolewa ndani, ikabidi niende kwenye gari langu nikapumzike  ili nisubiri sherehe ikiisha nikaonane na Diamond ili animalizie fedha yangu iliyobaki ambapo shilingi 625,000 ya matenti, 300,000 ya deni la awali na 80,000 ya usafiri ambapo jumla ni shilingi 1,005,000.”

MAMA DIAMOND AFUATWA, ASEMA NIVYO SIVYO

“Nikawa namfuata mama Diamond kumuulizia, akanijibu hovyo kwamba  tumewachefua sana, Esma naye akawa anatukimbia. Nikawaambia watu wangu tuondoke.

“Siku iliyofuata (Jumatatu) asubuhi nilirudi tena, nikaambiwa Diamond amesafiri. Cha ajabu mama yake akaniambia hakuna tunachodai na yale makapeti alinunua mwanaye.

ASHINDA NJE KWA DIAMOND

“Nilikaa pale nje kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa alasiri. Nikamwambia amuulize mwanaye kwenye simu ili nijue nini kinandelea, Diamond akajibu kwa kifupi tena kwa kutuma meseji kwamba si kwa upambaji ule na kusema kuwa, fedha aliyotupatia anaona inatosha.

“Mimi nilisema lazima nilipwe fedha zangu, Esma na mama yake wakaniambia mimi ndiye niwe ninakumbusha mara kwa mara, Diamond ni msahaulifu sana. Niliondoka, baadaye nilimtafuta meneja wa Diamond (Hamisi Tale ‘Babu Tale’) kwa sababu Diamond alikuwa hapokei simu yangu,” alisema Lutengano.

Meneja huyo aliendelea kusema kuwa, Babu Tale alimjibu yuko bize na bethidei ya mwanaye lakini baada ya siku chache alimuita akamwambia ameongea na Diamond akamwambia amemlipa fedha mara mbili lakini hajaridhika na upambaji wao na fedha aliyoitoa anaona imetosha hivyo hawezi kulipa zaidi (licha ya makubaliano).

MAMA DIAMOND ASAKWA

Kwa upande wake, mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu kifupi: “Hatudaiwi chochote waulize haohao waliokupa taarifa na namba zangu (akamalizia na tusi).”

SIMU YA DIAMOND HAIPOKELEWI

Simu ya Diamond ilipopigwa haikupatikana hewani muda wote, lakini Babu Tale yeye alisema hajui lolote kuhusu mapambo.

Leave A Reply