The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu wa Zamani wa Japan Afariki Dunia Baada ya Kupigwa Risasi

0
Waziri  Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi

WAZIRI  Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe aliyepigwa risasi mbili wakati akihutubia katika kampeni ya uchaguzi katika mji wa Nara, amefariki dunia, Shirika la NHK limeripoti.

 

Shambulio hilo dhidi ya Abe (67) limetokea katika Mji wa Nara, na inaripotiwa kuwa Mtuhumiwa ambaye ni Mwanaume aliye na miaka ya 40 amekamatwa.

 

Abe alikuwa waziri mkuu wa Japan mwaka 2006-07 na 2012-20 na anakuwa waziri mkuu aliyehudumu kwa kipindi kirefu zaidi nchini humo.

Leave A Reply