The House of Favourite Newspapers

Wakulima Iramba Wamshukuru Rais Samia kwa Kuwapa Mbolea ya Ruzuku

0

WAKULIMA wilayani Iramba mkoani Singida wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu huu wa kilimo ambayo wamekiri wameanza kuona matokeo ya ruzuku hiyo mashambani.

 

Wananchi hao wameyasema hayo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo wakati akiendelea na ziara yake mkoani humo kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mwaka 2020/25, kukagua uhai wa chama mashinani na kuzungumza na wananchi.

 

“Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa mbolea ya ruzuku, tumeona matokeo yake katika mashamba yetu, tumeona big result now (matokeo makubwa sasa),” amesema Peter Paulo, mkazi wa Iramba mbele ya Chongolo.

Leave A Reply