The House of Favourite Newspapers

Heche Atema Cheche Sakata la Kampuni ya Tanga Cement Kutaka Kuinunua Twiga Cement

0

Mwanasiasa maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ametema cheche kuhusu sakata linaloendelea la Kampuni ya Twiga Cement kutaka kuinunua Kampuni ya Tanga Cement.

Heche amesema jambo hilo litasababisha kuzidi kupanda kwa bei ya saruji na kuwa mzigo kwa wananchi.

Ameyasema hayo jijini Mwanza katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza kwamba mpaka sasa, Tanzania ndiyo inayoongoza kwa saruji kuuzwa bei ya juu kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.

Ameongeza kwamba kitendo cha Twiga Cement kuinunua Tanga Cement, kitaongeza ukiritimba katika soko la saruji nchini.

Leave A Reply