testiingg
The House of Favourite Newspapers

Balozi wa Ethiopia atua Mwanza, lengo ni kuwekeza

0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema ujio wa Balozi wa Ethiopia hapa nchini Shibru Mamo utazidi kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya Tanzania na Ethiopia kutokana na Mwanza kuwa na fursa nyingi za kiuchumi likiwemo Ziwa Victoria. Akizungumzia ujio wa Balozi huyo Ofisini kwake leo mara baada ya mazungumzo yao, Mkuu huo wa Mkoa amesema Ziwa Victoria kuna mazalia mengi ya samaki ambayo Balozi huyo atapata fursa ya kuona eneo lipi litakuwa mwafaka kiuchumi baina ya nchi hizo. Mnafahamu wenzetu wanaongoza kwa Ufugaji wa Ng’ombe Barani Afrika, na sisi ukanda huu tuna ufugaji pia hivyo tunaweza kubadilishana uzoefu katika eneo hilo pia Chuo Kikuu cha SAUT ni sehemu nzuri ya kubadilishana uzoefu wa mipango ya vyuo”  Makalla

“Nimefarijika kufika hapa Mwanza na nitatembelea maeneo ya Chuo Kikuu cha SAUT, Uhamiaji na Gereza la Butimba,yapo mambo nitakayojifunza ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zetu”, Mhe.Balozi Shibru Mamo. Ziara hiyo ya Balozi wa Ethiopia ni msisitizo wa ushirikiano aliosema Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu alipofanya ziara nchini Ethiopia.

 

Leave A Reply