The House of Favourite Newspapers

Katika Kuunga Mkono Juhudi Za Serikali, Oryx Gas Imeendelea Kuhamasisha Matumizi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania, Benoite Araman akielezea mchango wa Kampuni hiyo katika kufanikisha jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kuelekea mwaka 2032 wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu uwekezaji kwa maendeleo ya usawa na Jinsia unaoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum, DK Doroth Gwajima na kulia ni Waziri wa Jinsia Kilimo, Sanaa na Mali Kale kutoka nchini Kenya, Aisha Jumwa. Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Oryx Gas Tanzania Limited imeendelea umuhimu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama hatua za kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha nishati hiyo kuelekea mwaka 2032.

Hayo yameelezwa Novemba 15, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtedaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa mawaziri mbalimbali barani Afrika uliolenga kujadili uwekezaji kwa maendeleo ya usawa wa kijinsia.

Wakati wa mkutano huo ulihusisha mijadala malimbali ukiwemo haki wanawake na mtoto wa kike barani Afrika na suala zima la kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania, Benoite Araman (mwenye suti kushoto) akifurahia jambo na wadau kwenye mkutano huo.

Katika mijadala hiyo sekata binafsi pia zilishiriki ambapo kwa upande wa Oryx Gas Tanzania iliwakilishwa na Benoit Araman na kueleza hatua mbalimbali inazochukua katika kuwawezesha wanawake kiuchumu na kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Ningependa kushiriki hadithi hii ambayo inaweza kuhusishwa, sina hakimiliki kwenye hadithi hiyo, kwa hivyo jisikie huru kuileta nyumbani kwako katika nchi yoyote unayoishi, kwa sababu ninaamini tunaelekea katika njia ifaayo sana” anasema Benoit Araman

Pamoja na mambo mengine Araman anasema “Nitakuelezea jinsi gani kilo sita za LPG zinaweza kubadilisha maisha ili mtu aweze kubadilisha maisha.

“Kwa hivyo jambo la kwanza kabisa ambalo ningependa kukuambia, sina budi kukiri hilo kuwa Watanzania tunafanya vizuri sana katika suala la usawa maana mnavyojua serikali ya Tanzania inafanya vizuri sana katika masuala ya usawa wa kijinsia”

Amefafanua kuwa hata katika kampuni yao kuna uwakilishi mzuri wa wanawake, na hata dhima ya kampuni ni katika kumuwezesha mwanamke katika utumiaji wa nishati safi na hii ndiyo njia ya kwanza wanayotembea nayo.

Aidha amesema hana uhakika kwamba lazima jinsia ya kike wasizidi hamsini kwa hamsini lakini angependa kueleza katika Kampuni ya Oryx usawa wa kijinsia ni kipaumbele chao kikubwa.

Kwa upande wa ulinzi wa mazingira pia amesema wanafanya vyema zaidi katika kuboresha nishati ya kupikia kwa kuwa tunafanya vyema sana na tumekuwa tukisambaza mitungi ya gesi ya kupikia kwa jamii ya wakinamama nchini kote.

“Kwa hivyo kimsingi unapata kitu kutoka kwetu kuwa ndio waanzishaji wa harakati hizi za uhamasishaji wa suluhisho la matumizi ya nishati safi ya kupikia na hii ilianza kwa mazungumzo ya kawaida na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini na Bungeni.”

Leave A Reply