Waziri Jaffo Asema Kuimarika Kwa Sekta Binafsi Kutawezesha Kupanua Wigo La Ajira Nchini
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yakiwa yanaendelea Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Suleiman Jaffo amesema kuimarika kwa sekta binafsi kutawezesha kupanua wigo wa ajira kwa vijana wanaohitimu elimu ya juu hapa nchini.
Wazir Jafffo ameyasema Julai, 6 2024 wakati alipohudhuria Siku Maalum ya China iliyoambatana na maonesho ya 48 ya biashara ya kitaifa -Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar.
Akiwakaribisha wawekezaji kutoka China na mataifa mengine kuwekeza ili kukuza uchumi na kutoa ajira kwa vijana alisema;
“Taarifa zinaonesha kwamba zaidi ya dola za Marekani bil 3.3 tunasafirisha , lakini tunaingiza bidhaa kutoka China ambazo thamani yake ni zaidi ya shilingi trilioni 3.5,”amesema.
Amesema Tanzania na China zinauhusiano wa muda mrefu ambayo yemeleta faidi katika nchi hizo hasa katika uchumi kwa kusafirisha bidhaa.
Ameongeza kuwa uhusiano mwingine upo kwenye viwanda vya wachina ambavyo vimejengwa hapa nchini na kutoa ajira nchini,ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa kufanya kazi ya ukandarasi.
Amesema kampuni 100 zimeweza kushiriki katika maonesho hayo ua 48 ya biashara ya kimataifa. “Makampuni hayo yametoka China, hii tunavutia uwekezaji katika nchi yetu, binafsi kama Serikali imeamua inaweka mazingira wezeshi kuhakikisha wawekwzaji wanapata fursa ya kuwekeza nchini,”amesema.
Dk. Jaffo amehamasisha kuendelea kwa ushirikiano huo na kuwekeza ili kukuza uchumi ili kuongeza ajira kwa vijana haswa wanaomaliza elimu ya juu na vyuo kati hapa nchini.
Alimalizia kwa kusema kundi kubwa la vijana hapa nchini haliwezi kupata ajira lote serikalini hivyo sekta hizo ndizo zitakazokuwa msaada.