Jubilee Health Insurance Yazindua Huduma Mpya ya FBiz
Kampuni ya Bima ya Jubilee Health Insurance imezindua huduma mpya ya FBiz, ambayo imeundwa mahsusi kwa ajili ya Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SMEs) wenye wafanyakazi 3 hadi 15. Huduma hii inalenga kutoa chaguo za bima zinazoweza kubadilishwa, zikilenga mahitaji ya familia na bajeti mbalimbali.
FBiz imejipambanua kwa kutoa suluhisho linalobadilika na linalomudu gharama, hivyo kuwawezesha wamiliki wa biashara ndogo kutoa bima bora ya afya kwa wafanyakazi wao huku wakikabili changamoto za kifedha. Bidhaa hii mpya inalenga kutoa manufaa ya familia, huduma za afya za kina, na upatikanaji wa mtandao mpana wa watoa huduma za afya.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Uendeshaji wa Jubilee Health Insurance, Shaban Salehe, alielezea furaha yao kwa kuzindua FBiz na kutoa suluhisho la bima ya afya ambalo ni nafuu.
“Lengo letu ni kusaidia ukuaji na mafanikio ya biashara ndogo kwa kutoa bidhaa inayokidhi mahitaji yao maalum huku ikiboresha afya na ustawi wa wafanyakazi wao na familia zao,” alisema Salehe.
Jubilee Health Insurance imejidhihirisha katika uvumbuzi na kuridhisha wateja, jambo ambalo linaonekana wazi katika maendeleo ya bidhaa ya FBiz. Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kushughulikia mahitaji yanayobadilika ya sekta ya afya nchini Tanzania, na unaonesha zaidi dhamira ya Jubilee Health Insurance kutoa suluhisho za bima ya afya za ubora wa juu na zinazopatikana kwa urahisi.
www.jubileetanzania.co.tz @jubileehealthtanzania