The House of Favourite Newspapers

Chikukupi Ajitosa Kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki

0

Kada wa Chama Cha Mapinduzi  Chikukupi Njelu Kasaka amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe 14.08.2024. Kada huyo amechukua fomu katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo jijini Dodoma akisindikizwa na makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.

Chikukupi Njelu Kasaka ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili ni mbobezi wa masuala ya siasa, utawala na diplomasia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mahusiano ya kimataifa na diplomasia.

Chikukupi amekitumikia Chama Cha Mapinduzi katika nyanja tofauti na pia ni mjumbe katika kamati mbalimbali. Baada ya kuchukua fomu hiyo Chikukupi Kasaka akiongea na waandishi wa habari ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kukuza umoja na uchumi katika Jumuia ya Afrika Mashariki.

Chikukupi ameahidi kuindeleza kazi hiyo ili kuiwezesha nchi yetu kupiga hatua kiuchumi kwa  kuimarisha uchumi na fursa kwa vijana na taifa kwa ujumla.

Leave A Reply