Wamiliki wa Shule Binafsi Sasa Kuchagua Benki Au Tigo Pesa Kwenye Malipo ya Ada
Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo kwa kushirikiana na ZMotion wameendesha mafunzo ya siku moja kwa wamiliki na Wakurugenzi wa shule binafsi kuhusu huduma mpya ya Lipa Ada.
Mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam yamelenga kuhakikisha kunakuwa na ufanisi wa mfumo huo mpya ambao unatoa fursa kwa wazazi na walezi kulipa ada kidogo kidogo kulingana na uwezo wao.
Mkurugenzi wa Biashara wa Tigo Pesa, James Sumari amesea mfumo wa ‘Lipa Ada’ ni mojawapo ya ubunifu wa kiteknolojia uliolenga kutatua changamoto zinazowakumba wazazi na walezi na shule katika suala la ulipaji ada na kusema kuwa malipo kupitia mfumo huo yatakuwa yakifanyika kupitia huduma ya Tigo Pesa, hivyo kurahisisha mchakato mzima.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ZMotion, Said Ally alibainisha kuwa mfumo wa Lipa Ada umesanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya shule binafsi na ni rahisi kutumia.