Taifa Stars kusaka alama 3 leo dhidi ya DR Congo

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itashuka dimbani leo kusaka alama 3 muhimu dhidi ya Timu ya Taifa ya DR Congo katika mchezo wa Kundi H kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Taifa Stars wanashikilia nafasi ya pili katika msimamo kwa kundi hilo wakiwa na alama 4, huku wapinzani wao DR Congo wakiwa kileleni na alama 9 huku sare yeyote katika mchezo huu itawapa tiketi ya kufuzu katika michuano hiyo.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia majira ya 10:00 alasiri huku Taifa Stars, baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa 1-0 Oktoba 10 kule DR Congo, leo watakuwa na kibarua cha kutafuta ushindi utakao wasaidia na kuendelea kuweka hai matumaini ya kufuzu michuano hiyo kwani ushindi huo utawasaidia kufikisha alama 7 zitazowahakikishia kusalia nafasi ya pili katika kundi hilo bila kuathiriwa na matokeo yeyote yatakayopatikana katika mchezo mwingine wa kundi hilo utakaozikutanisha Timu ya Taifa ya Ethiopia dhidi ya Timu ya Taifa ya Guinea majira ya saa 4:00 usiku leo.