The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi wa Dar24 Media Maclean Mwaijonga Apatikana – Video

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kufuatia taarifa ya kutofahamika alipo mtu mmoja aitwaye Maclean Mwaijonga, mfanyakazi katika kampuni ya DATA VISION INTERNATIONAL LTD, Mikocheni Rose Garden Kinondoni, tarehe 2 Novemba, 2024 saa 12 jioni zilipatikana taarifa kupitia kwa ndugu yake mmoja kuwa mtu huyo ameonekana maeneo ya Kigamboni. Polisi wakiwa na ndugu zake walienda mpaka maeneo ya Kigamboni, Buyuni na kumkuta mtu huyo akiwa barabarani.
Alikuwa anapepesuka, walimpeleka hospitali na baada ya vipimo ilionekana ana afya njema. Mtu huyo anadai kuwa alichukuliwa na watu aliokuwa na mazunguzo nao ya kibiashara kwa muda mrefu, ambapo kitu anachokumbuka walimpa kinywaji kilichomfanya apoteze fahamu mpaka alipopata fahamu na kujikuta eneo alipopatikana.
Jeshi la Polisi linawashukuru watu wote kwa ushirikiano wao walioutoa uliopelekea kupatikana kwake. Uchunguzi zaidi unaendelea.

Imetolewa na;
Muliro J. MULIRO – SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam