Rais Samia Afanya Mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Ikulu, Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 12 Novemba, 2024 amefanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda kwenye Kikao maalum cha maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.