Benki ya Absa Tanzania Yashinda Tuzo 11 za Heshima Mwaka 2024

Utendaji bora wa Benki ya Absa Tanzania mwaka 2024 umeoneshwa kupitia matokeo yake mazuri ya kifedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Mapato ya jumla yaliongezeka kwa 25% kufikia TZS bilioni 105, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa 65% kufikia TZS bilioni 54. Amana za wateja ziliongezeka kwa 21%, zikionesha uimara wa benki hiyo na uwezo wake wa kutoa ukuaji endelevu.
Tuzo ya Chapa ya Benki Inayokua haraka zaidi inaadhimisha maendeleo makubwa ya Benki ya Absa Tanzania tangu ilipoanzishwa mwaka 2020. Ndani ya miaka minne tu, Absa imepata kiwango sawa cha imani na kutambuliwa kama benki za ndani na kimataifa zenye karibu karne moja ya historia nchini Tanzania.

Tuzo hii inaonyesha ahadi ya chapa ya Absa: ‘Stori yako ina Thamani’, inadhihirisha kujitolea kwa benki hiyo katika kuthamini Stori za kipekee za wateja wake, kuunda suluhisho za kibunifu, na kuiwezesha jamii.
Tuzo ya Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha inaonyesha dhamira ya Absa katika kukuza ujumuishi wa kifedha. Kupitia bidhaa kama Akaunti ya Absa She Business, benki hiyo imewawezesha wanawake wajasiriamali kupata huduma za kibenki bila gharama, msaada wa ushauri, na programu za kujenga uwezo.
Katika sekta ya SME, suluhisho maalum za Absa na ushirikiano wa kimkakati zimesaidia benki kushinda tuzo ya Benki inayotoa huduma Kwa wateja wadogo na wa Kati (SME) inayokua haraka zaidi Tanzania 2024.

Tuzo ya Benki ya Wateja Rejareja inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 inaonyesha msisitizo wa benki hiyo katika mabadiliko ya kidijitali na urahisi wa wateja, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa huduma za uwakala na suluhisho za kibunifu kama jukwaa la malipo la Mobi Tap.
Kutambuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji kama MD/CEO wa Mwaka na tuzo ya Ripoti Bora za Kifedha 2023 kunathibitisha kujitolea kwa Absa kwa utawala bora, uwazi, na uongozi wa mfano wa kuigwa.
Tuzo kutoka Consumer Choice Awards, kama Benki Inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu wa Mikopo Tanzania, zinaonyesha dhamira ya Absa ya kuwapa wateja nafasi ya kwanza katika shughuli zake.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema:
“Tuzo hizi ni ushahidi wa nguvu ya ushirikiano wetu na wateja na wadau wetu. Tunaheshimika kutambuliwa katika nyanja nyingi, na tutaendelea kujitolea kuimarisha Afrika ya Kesho kupitia suluhisho za kibenki zenye ubunifu, ujumuishi, na athari chanya.”
Benki ya Absa Tanzania inapoendelea na safari yake ya ukuaji na mabadiliko, inabaki imara katika dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwawezesha jamii. Tuzo hizi ni kielelezo cha kujitolea kwa benki hiyo kwa uvumbuzi, uwazi, na kuridhisha wateja wake.

