The House of Favourite Newspapers

Usikose Semina Hii ya Fahamu Talk 2016

0

mauki123

Dk. Chris Mauki.

Ni watu wengi sana wakiwemo vijana wanaingia kwenye mahusiano bila ya ufahamu wa kutosha na baadaye kwa kukosa ufahamu huo wanakutana na changamoto wasizoweza kuzikabili na hivyo kufeli katika mambo mengi ikiwemo kwenye ndoa zao na hususani katika shughuli zao za kiuchumi na kimaisha kwa sababu ya ukweli kwamba mahusiano yanasababisha msongo mkubwa wa mawazo na hivyo waathirika wanapunguza uwezo wao wa kufikiri katika kazi zao za kila siku na hivyo kuathiri uchumi wao.

Luvanda

Anthony Luvanda.

Ni ukweli kwamba mara nyingine hali zetu za kiuchumi pia zinaweza kuathiri baadhi ya mambo kwenye mahusiano yetu. Pande zote hizi mbili zinahusiana kwa karibu sana. Hili ndilo kusudi maalumu la magwiji hawa wawili kuamua kuungana pamoja kupaza sauti kupitia Fahamu Talk.

Dk. Chris Mauki mtaalamu wa Saikolojia na mahusiano akiongelea mambo ya kujenga mahusiano na Anthony Luvanda mjasiriamali na mhamasishaji akidadavua mambo muhimu ya kuboresha uchumi binafsi.

Fahari Talk

Fahamu talk itafanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 4 Septemba kuanzia saa 6 mchana. Kwa sababu kubadilika ni uamuzi binafsi hivyo basi tunawasisitiza wale wenye kiu ya mabadiliko kutokukosa tukio hili muhimu maishani.

Tunawashukuru sponsors wote kwa kutuwezesha kufanikisha hili. Shukrani za dhati ziende kwa PSPF, UTT, Cocacola, Cops Security Global Publishers, Kilimanjaro Audiovisual, 8020 Fashion, Jamii Forums, Magazeti ya Mtanzania na Mwananchi, Dar Insights, Fortune Studios, CYN Henjewele Docorations, JRoc Moda na Clouds FM.

Sisi tunasema FAHAMU TALK, JITAMBUE, PANUA UPEO WAKO.

Leave A Reply