The House of Favourite Newspapers

900 Itapendeza Kumbe ni Shabiki wa Chelsea

0
Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo (kushoto) akiwa na Dk Shika

 

MSOMI na ‘bilionea’ aliyejipatia umaarufu hivi karibuni baada ya kutaka kununua nyumba za mnada za mfanyabiashara, Said Lugumi, Dk Louis Shika amefunguka kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Klabu ya Chelsea ya jijini London, England.

 

Dk Shika amepata umaarufu hivi karibuni baada ya kutaka kununua nyumba katika mnada kisha kushindwa kulipa fedha kwa wakati hali iliyosababisha ashikiliwe na polisi kwa kuharibu mnada.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Shika alisema kuwa amekuwa hafuatilii masuala ya soka mara kwa mara hasa la hapa nyumbani Tanzania.

“Mimi sifuatilia sana masuala ya mpira hapa nyumbani, hivyo nashindwa kuzungumzia timu za hapa nitakuwa muongo lakini Ulaya mimi ni shabiki wa Chelsea, naipenda.

“Mara nyingi napenda kufanya mambo yangu binafsi, ndiyo maana unakuta nakosa hata muda wa kufuatilia sana masuala hayo ya michezo,” alisema Shika.

Stori; Martha Mboma, Championi Ijumaa

Leave A Reply