Mwanamke Ateseka Kwa Uvimbe Mkoa Wa Mara
Bi Nchagwa Marwa, mkazi wa Kijiji cha Korotambe, Kata ya Mwema Tarafa ya Inchugu Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, anateseka na ugonjwa uliodaiwa kuwa ni kansa tangu mwaka 2004.
Bi Nchagwa analia na umaskini, na kuolewa ‘nyumba ntobhu’ yaani ndoa ya jinsia moja hasa alivyokutwa na ugonjwa huo unaosababisha kushindwa kula na kuongea.
Akifafanua zaidi Nchagwa alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi muda wote natokwa na machozi, ninashindwa kupata fedha ya kwenda kutibiwa ugonjwa huu Hospitali ya Bugando iliyopo Mwanza. Huwa nashindwa kupata usingizi kutokana na maumivu ya ugonjwa huu hadi kujutia kuzaliwa duniani kutokana na kukata tamaa pale nilipoambiwa kuwa matibabu yake huchukua gharama kubwa katika hospitali niliyoandikiwa barua na madaktari wa Hospitali ya Halmashauri ya Tarime.
“Namtegemea Mwenyezi Mungu na Watanzania lakini kipekee namuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli na serikali yake inisaidie gharama za matibabu.Nilifanikiwa kuchangiwa na madiwani wa Tarime na watumishi wa ofisi ya mkuu wa wilaya shilingi 220, 000, Agosti 24, mwaka huu.
“Hatua hiyo ilikuja baada ya madiwani wa kata yangu, Mwema Petrues Itaara na wa Viti Maalum, Victoria Kegoye kunifikisha kwa madiwani wenzao wakiniombea mchango wa matibabu.
Nawashukuru lakini fedha hiyo haitoshi kwa matibabu yangu na ndiyo maana naomba msaada kwa Watanzania wenzangu. Nawaomba ili kunusuru maisha yangu.”
Kwa yeyote aliyeguswa na mateso ya bibi huyo amsaidie kwa kutumia namba ya diwani Victoria Kegoye ambaye pia ni ndugu yake kupitia namba 0769185652. Mtoto Teckla unaweza kumsaidia kwa namba ya mama yake 0787020034.
Comments are closed.