The House of Favourite Newspapers

WEMA, BWANA MPYA SIRI NJE!

DAR ES SALAAM: Siri njee! Baada ya ukimya wa muda mrefu kupita huku tetesi zikisambaa kuwa mrembo Wema Sepetu amezama kwenye penzi na mfanyabiashara Lawrence Masanja ‘R.a.h.u.r’, Ijumaa limeingia mzigoni na kuibua kila kitu kuhusiana na uhusiano wa wawili hao huku wenyewe wakifunguka kinagaubaga.

MAMBO YALIANZA HIVI

Awali, tetesi za uhusiano wa Wema na R.a.h.u.r zilianza kuibuka miezi kadhaa iliyopita kwenye mtandao wa Instagram baada ya Wema kuibuka mshindi wa Muigizaji Bora wa Kike na Chaguo Bora la Watu kupitia tuzo zilizofahamika kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF).

UJUMBE WENYEWE

Mara baada ya mrembo huyo kuibuka kidedea, R.a.h.u.r akaposti picha ya Wema kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza na ujumbe uliosomeka hivi: “People’s choice & Best Actress, Ni category kubwa sana. Hongera kwa ushindi huo, you deserve, i’m proud of you. #Maso.”

WEMA NAYE AKAJIBU

Baada ya ujumbe huo, Wema alimjibu kwa ujumbe wenye viashiria vya kimahaba ambao ulileta gumzo kubwa mitandaoni huku wengi wakijiuliza kwamba ni wapenzi au nini kinaendelea kati yao.“I’m glad i made you proud my love. It won’t stop, I promise you.”

MITANDAONI KWACHAFUKA

Majibu hayo ya Wema kwenda kwa Rahur yaliibua gumzo la aina yake ambapo kila mmoja alionesha mtazamo wake na jinsi alivyoelewa.

Kuna ambao walikwenda moja kwa moja na kumpongeza Wema kwa kupata mpenzi mpya kwani hawajawahi kumuona ana mwanaume mwingine tangu amwagane na yule kigogo, Bakari Kila aliyedakwa na madawa ya kulevya nchini Kenya.

Wengine walipinga kwa kusema kuwa kumuita mtu baby haimaanishi kuwa ni mpenzi wake kwani siku hizi hata marafiki wa kawaida wanaweza kuitana baby. “Jamani siku hizi mtu kukuita baby sio ishu, mtu anaweza kuwa na marafiki wengi tu wa kiume na wote akawa anawaita baby kwa nyakati tofauti,” ilikuwa ni moja ya maoni ya mmoja wa wachangiaji.

MARA PAAP, MAUA!

Baada ya muda kidogo kupita tangu jamaa huyo ampongeze kwa ushindi wa tuzo, R.a.h.u.r alitupia kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya maua, ambayo ndani ya muda mfupi, Wema naye aliyaposti tena katika ukurasa wake na kuandika ujumbe kwamba anampenda sana mshkaji huyo.

GRASI ZA JUISI

Kama hiyo haitoshi, mwishoni mwa wiki iliyopita wakati ulimwengu wa watu wa mtandaoni ulipokuwa bize na msiba wa muigizaji Rose Alphonce ‘Muna’, Patrick, R.a.h.u.r akakinukisha tena kwa kuposti picha ya mikono miwili iliyoaminika kuwa mmoja ni wake na mwingine ni wa Wema huku ikiwa imefunikwa na alama ya kopa.

Mikono hiyo aliyoiposti kwenye Instagram kupitia kipengele kiitwacho Your Story, ilionekana imeshika grasi za juisi huku gumzo likiibuka juu ya mkono uliosemekana ni wa Wema kwa watu kuoanisha na picha zake mpya zilizomuonesha akiwa na baibui jeusi na kucha za rangi ya pinki.

GUMZO LA MOROGORO

Mapema wiki hii, R.a.h.u.r aliibua gumzo lingine kwa kuonesha picha ya fedha na kuelekeza mashabiki wake kuwa anaelekea Morogoro ambako inaaminika Wema pia atakuwa mkoani humo kwa ajili ya mashindano ya urembo yanayotarajiwa kufanyika wikiendi hii. Hapo napo, wafausi wa mtandao huo waliunganisha ‘doti’ na kusema kuwa kwa matukio hayo yote, Wema atakuwa ana uhusiano na jamaa huyo.

R.A.H.U.R. ANASEMAJE?

Kutokana na ushahidi huo na maoni ya watu kusema wawili hao ni wapenzi, Ijumaa liliamua kumtafuta R.a.h.u.r ili aweze kuzungumzia juu ya uhusiano wake na Wema ambapo alipopatikana na kuulizwa hakutoa jibu la moja kwa moja. “Kiukweli mimi huwa sipendi media,” alijibu. Alipoendelea kubanwa zaidi, aliingia mitini.

HUYU HAPA WEMA

Ijumaa lilimsaka Wema ili kumsikia anazungumziaje uhusiano huo ulioonekana kupendwa na mashabiki, alipopatikana alisema kuwa watu wajue tu kuwa jamaa huyo ni mshkaji wake. “Mimi huyo ni mshkaji wangu tu wala hakuna kinachoendelea,” alijibu Wema.

AISHIA KUCHEKA

Wema alipoulizwa juu ya kumuandikia mshikaji huyo ujumbe wa mahaba mara kwa mara alicheka na kukata simu. Hata hivyo, mmoja wa watu wa karibu wa Wema aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, wawili hao kuna zaidi ya urafiki kati yao ila wenyewe wamekuwa wasiri sana.

“Naomba usinitaje gazetini maana si unajua tena mimi na yeye (Wema) tukoje, ila kiukweli wanapendana na ninachoona mimi hawataki watu wajue, wafuatilieni kuna siku mtawanasa tu ila mimi natamani sana waoane, wanaendana sana,” alisema sosi huyo.

TUJIKUMBUSHE

Wema mwenye kismati cha kupendwa na watu, kwa muda mrefu amekuwa akifuatiliwa na kuungwa mkono na mashabiki wake kila anapoanzisha uhusiano mpya. Mashabiki hao walimpa ushirikiano kwa nyakati tofauti alipokuwa na uhusiano na wanaume tofauti wakiwemo, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Mshiriki wa BSS, Idris Sultan.

STORI: MEMORISE RICHARD, IJUMAA

Comments are closed.