DUDE: Wanangu Wanapata Taabu Sana!

MWIGIZAJI mahiri wa Tamthiliya ya Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa hakuna kitu kinachomuumiza kama watoto wake wakija kumuambia wanawaita watoto wa tapeli.

 

Dude ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kila mara watoto wake wanakuja kumshtakia kuwa wenzao Shilole wanawatania baba yao ni mwizi, jambo ambalo amekuwa akitumia muda mrefu kuwaelewesha kuwa ni kazi na siyo kweli kama wanavyowatania.

 

“Unajua nina watoto wakubwa wanaonielewa lakini wadogo wanaumia sana wakiwatania kuwa baba yao ni tapeli na wakija kushtaki kwangu, naumia ila najikaza na kuwaambia ile ni kazi kama ilivyo kazi nyingine hivyo wasiyabebe wanayoambiwa na wenzao,” alisema Dude.


Loading...

Toa comment