The House of Favourite Newspapers

A-Z Makambo alivyosaini Horoya AC

STRAIKA wa Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo, jana alfajiri alirejea nchini akitokea Guinea alipokwenda kusaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea Horoya AC.

 

Taarifa zilianza kuzagaa juzi Alhamisi jioni kwa baadhi ya picha zikimuonyesha Makambo akisaini na nyingine akitambulishwa na viongozi wa Horoya huku akiwa amevalia jezi yenye rangi nyekundu na nyeupe. Mara baada ya picha hizo kuzagaa, Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alithibitisha kuondoka kwa Makambo nchini akiongozana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

 

Championi Jumamosi linakupa A-Z safari ya mshambuliaji huyo alipokwenda Guinea kwa ajili ya kusaini mkataba. Jumanne usiku aondoka Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti hili, Mkongomani huyo aliondoka nchini usiku wa Jumanne iliyopita mara baada ya kumaliza mchezo wa ligi na Ruvu Shooting ambao Yanga ilishinda bao 1-0.

 

Mshambuliaji huyo akiwa uwanjani katika mchezo huo wa Ruvu, kumbe alikuwa anaijua vizuri safari hiyo ya Guinea kabla ya usiku wake kuondoka pamoja na kocha wake baada ya kuomba ruhusa kutoka kwa viongozi wake.

Mkataba wake na Yanga wazua maswali Baada kusaini mkataba huo, mengi yalijitokeza kati ya hayo ni juu ya mkataba wake na Yanga kuwa, alisajiliwa Jangwani kwa mkopo akitokea Motema Pembe ya DR Congo.

 

Jingine ni kuwa, mshambuliaji huyo hakumaliziwa fedha zake katika mkataba wake wa miaka miwili aliosaini Yanga, pia madai yake ya mshahara wa miezi minne ambayo kwa mujibu wa kanuni za Fifa mchezaji huyo ni huru kwani mchezaji asipolipwa mshahara ndani ya miezi mitatu klabu itakuwa imevunja mkataba.

 

Msolla alilitolea ufafanuzi hilo kwa kusema kuwa: “Makambo bado mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili unaomalizika 2020, hivyo mashabiki waondoe hofu katika hilo na fedha zitakazopatikana zitaingia klabuni.”

 

 

Viongozi wakana mkataba Horoya Picha mbalimbali zikiendelea kusambaa mitandaoni zikimuonyesha Makambo akisaini Horoya, viongozi wa Yanga walijitokeza na kuanza kukanusha kupitia vyombo vya habari kwa kusema kuwa mshambuliaji huyo alikwenda Guinea kwa ajili ya vipimo vya afya. “Uongozi unachofahamu kuwa, Makambo alikwenda nchini huko kwa ajili ya vipimo pekee na siyo kitu kingine na baada ya vipimo akatakiwa arejee leo (jana Ijumaa) na kweli tayari ametua nchini alfajiri pamoja na kocha.

 

 

“Hivyo, baada ya kurejea nchini Kamati ya Utendaji ya Yanga imepanga kukutana na kocha Zahera leo (jana) usiku ambaye yeye aliongozana na mchezaji huyo kwa ajili ya kutupa taarifa zaidi kuhusu walipofikia katika mauzo yake na baadaye kutolea taarifa za kuuzwa kwake.

 

“Kikubwa tutakachokiangalia kwa Makambo ni maslahi pekee ndiyo yatakayomuachia, kwani tayari mshambuliaji huyo ana ofa nne nzuri kutoka nchi za Afrika zilizoonyesha nia kubwa ya kumsajili baada ya kuvutiwa na kiwango chake. “Mashabiki wa Yanga yasitishike kumuona Makambo akiwa amevalia jezi za Horoya akiwa na viongozi, hilo limeshawahi kutokea kipindi cha nyuma lakini mchezaji haendi huko, ndiyo itakavyojitokeza kwa Makambo. Kumbe ana ofa ya Ulaya!

 

“Kati ya ofa nne alizozipata Makambo, mbili ni nchi za Afrika na mojawapo hiyo ya Horoya ambayo ilikuwa ya kwanza na nyingine ni kutoka nchi za Ulaya majina yao ni siri, nitaweka wazi baada ya dili kukamilika. Ishu ya kuuzwa kwa Sh Mil 223 Wakati mabosi wa Yanga wakikanusha kutouzwa kwa Makambo, taarifa zipo kuwa mshambuliaji huyo ameuzwa Horoya kwa dau la Sh Mil. 223 akisaini mkataba wa miaka mitatu.

 

“Makambo bado hajauzwa rasmi, uongozi unachofahamu mshambuliaji huyo alikwenda nchini huko kwa ajili ya vipimo vya afya na baada ya hapo ndiyo tutakaa meza moja na klabu hiyo na kuanza mazungumzo.

 

Makambo, Zahera warejea kimyakimya Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti hili, mshambuliaji huyo na kocha wake Zahera walirejea nchini jana Ijumaa saa kumi kamili alfajiri kimyakimya wakitokea Guinea alipokwenda kusaini mkataba.

 

Mara baada ya kutua nchini, kila mmoja alikwenda nyumbani kwake na kushindwa kujiunga na mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam. K

 

umbe alitumiwa tiketi ya ndege na Zahera Siri kubwa imefichuka ni kuwa, kabla ya kuondoka Makambo, mazungumzo ya kwenda kusaini mkataba huo, Klabu ya Horoya ndiyo iliwatumia tiketi za ndege Zahera na Makambo za kwenda na kurudi. Zahera alikwenda huko kama mwakilishi wa Yanga ambaye yeye atasimamia mauzo yote ya mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

 

Zahera aahidi kushusha mastraika zaidi yake “Kocha ametuhakikishia kuleta washambuliaji wazuri zaidi ya Makambo katika kuelekea msimu ujao na tayari ana orodha ya majina ya wachezaji hao anaowahitaji kuwasajili.

 

Zahera, Makambo watafutwa hawapokei simu Mara baada ya Championi Jumamosi kupata taarifa za kurejea kwa Makambo na Zahera liliwatafuta kwa njia ya simu ambazo ziliita bila ya mafanikio ya kupokelewa na walipotumiwa ujumbe kwa njia ya simu hawakujibu chochote. Siyo kawaida kwa Zahera kutopokea na kutoa ushirikiano kwa waandishi.

Comments are closed.