The House of Favourite Newspapers

A-Z Mr. Nice kulishwa sumu

0

NICEMsanii aliyewahi kubamba kwa staili ya Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu), Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ akiugulia.

Chande Abdallah

MASIKINI! Msanii aliyewahi kubamba kwa staili ya Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu), Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu hali iliyosababisha akimbizwe hospitali na kulazwa. Amani lina mkanda mzima.

MrNiceMr. Nice

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na staa huyo aliyewahi kubamba na nyimbo nyingi zikiwemo Kikulacho na Fagilia, Mr. Nice alikuwa Kahama, Shinyanga katika kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli.

“Ujue tangu Lembeli (James) yupo Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mr. Nice alikuwa mmoja wa watu wake wa karibu katika kumfanyia kampeni na kwa kipindi hiki ambacho Lembeli yupo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekuwa akiambatana naye kwenye kampeni. Kwa hiyo kulishwa kwake chakula chenye sumu huenda ni bahati mbaya,” kilisema chanzo.

Amani lilimvutia waya Mr. Nice, kujua zaidi hali yake ambapo alikataa kuweka wazi suala hilo kwa sasa kutokana na washauri wake kumsihi hivyo kwa kipindi hiki alichokuwa nacho.

Naye rafiki yake wa karibu aliyewahi kuingia naye katika malumbano, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ aliweka wazi kwa sasa hana mawasiliano na Mr. Nice lakini mwaka 2010 alifanya naye kampeni hukohuko Kahama za Lembeli.

Alipotafutwa Lembeli kuongea juu ya hili tukio, simu yake iliita bila kupokelewa.

Hivi karibuni, Mr. Nice kupitia mtandao wake wa Facebook, aliwashukuru mashabiki, familia na madaktari wake pamoja na Lembeli waliopigania kuokoa maisha yake.

Leave A Reply