The House of Favourite Newspapers

Ababuka uso kisa, vipodozi

0

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Mwajuma au mama Sauda, mkazi wa Vingunguti Mnyamani, Dar hivi karibuni yamemkuta makubwa baada ya kubabuka uso wake wote kutokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali.

Tukio hilo lililoibua gumzo katika mtaa huo na mitaa ya jirani, lilishuhudiwa pia na Mzee wa Hekaheka akiwa kwenye majukumu yake na alipowauliza mashuhuda kuelezea kilichotokea walikuwa na haya ya kusema;
“Huyu mama kiukweli alikuwa amezidi na haya yaliyomkuta atakuwa amejifunza. Wewe mtu gani anatumia mavipodozi ya kemikali kama chakula! Yaani vidonge, vipodozi vya maji anachanganya kwenye rosheni na matakataka mengine kibao!” Huyo alikuwa ni mama Subira akikandia.
Hata hivyo, japo mama Sauda aliyekutwa na hekaheka hiyo, baada ya mumewe kupewa taarifa na kufika, hakutoa msaada wowote zaidi ya kumshushia kichapo mkewe na kumtimua nyumbani kwake.

Leave A Reply